TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA?

Sera ya Raisi wetu wa Awamu ya Tano ya TANZANIA YA VIWANDA inatupelekea watanzania kuamka na kuanza kujiandaa katika shughuli kubwa tuliyonayo ili tufikishe lengo la kuwa na viwanda.Malengo yenye sera ya HAPA KAZI TU yanabidi yaendane na kazi kwa akili na auchunguzi wa hali ya juu kwa kile mheshimiwa anachohitaji kikamilike .

Watanzania hawataweza kufikia lengo la Tanzania ya viwanda endapo Swala la Mazingira halitoangaliwa kipindi cha uandaaji na uanzishwaji wa viwanda hivyo,Mabadiliko ya Tabia ya Nchi  yanayotokea hivi sasa yanachangiwa sana na uharibifu wa Mazingira,Kutotunza mazingira yetu kutasababisha kukosekana kwa malighafi ambazo zitatumika katika viwanda kwa ajili ya uzalishaji,Kutokuwepo kwa mvua kutapelekea kuwepo kwa njaa ambapo utendaji wa kazi za uzalishaji utapungua na gharama ya vyakula kupanda .Uchumi wetu hautegemei viwanda tu bali mazingira bora.Utunzaji wa mazingira si jukumu la raisi pekee  na wala hatupaswi kusubiri tamko kutoka kwa raisi  kukazia utunzaji wa mazingira yetu ili kutimiza malengo yetu ya kutokomeza umaskini na Kuinua uchumi wa Nchi

Tanzania ya viwanda ni ile itakayoipa kipaumbele Utunzaji wa Mazingira na Rasilimali zetu kwa ajili ya leo na Kizazi cha viwanda,



Previous
Next Post »

Toa maoni ili tuweze boresha huduma za taarifa zetu na sio matusi Tafadhari
EmoticonEmoticon