ELIMU YA MAZINGIRA YAWAFIKIA WANAKIJIJI WA KANYEGERE




Timu ya watoaji elimu ya mazingira ya Ecosafety and Conservation Organization (ECO) wakitoa elimu ya mazingira katika kijiji cha Kanyegele kilichopo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya .Watoaji wa elimu hiyo walikua wakifundisha juu ya utumiaji wa mbinu za asili katika kutunza mazingira yao na kuwa na matumizi mazuri juu ya rasilimali zao ikiwemo Vyanzo vya maji,misitu,na ardhi pia kupunghuza shuughuli za ukataji wa mikaa ambazo huchochea mabadiliko ya nchi. 

Timu hiyo ya wahamasishajji na watoa elimu walipata muda wa kuwauliza maswali wananchi hao kuhusu uelewa wao juu ya mazingira .Baadhi ya wanakijiji hao walisema ni mara yao ya kwanza  kupata elimu hiyo kwani ni wawakilkishi tukatika kata  ndio ambao hua wakihuduria na sio wote .Wanakijiji walishukuru sana kufikiwa  wakiwa katika makundi tofauti na kuipata elimu hiyo kwa pamoja,

Mkurugenzi wa Ecosafety and conservation organization(ECO) aliahidi kuwa yeye na timu yake ya  utoaji elimu ataboresha na kubuni  njia mbali mbali ya kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa  na kupata elimu hiyo ya mazingira ili mbinu za asili ziweze kutumika katika uhifadhi wa mazingira

0

Almasi akitoa utambulisho kwa wanakijiji na wataalamu wa mazingira


 wanakijiji wa Kanyegere wakifundishwa mbinu mbali mbali za  asili za utunzani mazingira

wanakijiji wa Kanyegere wakisikiliza kwa makini juu ya mbninu za utunzaji mazingira
Latest
Previous
Next Post »

Toa maoni ili tuweze boresha huduma za taarifa zetu na sio matusi Tafadhari
EmoticonEmoticon