MWANAMKE NA MAZINGIRA








kuna mahusiano makubwa ambayo viumbe vimeunganishwa katika kutegemeana .Leo nitazungumzia kuhusu Muuunganiko uliopo kati ya Mwanamke na Mazingira.WAtaalam na wanafalsafa wa (ECOFEMINISM) wanaamini kwamba mazingira na Mwanamke wanamahusiano wa asili kupitia shughuli anazozifanya mwanamke kuhakikisha anapata huduma zilizo muhimu  kwa familia na jamii kwa Ujumla .Vyanzo vya maji vinapokauka humradhimu mwanamke kutembea umbali mrefu ili kupata maji kwa ajili ya familia na shughuli za ujenzi kwa ajili ya maendeleo.Katika huu muunganiko ni dhahiri kwamba Mwanamke ana uhusiano ambao ni wa asilia.sasa tunafanyaje ili kutomuumiza mwanamke katika ikolojia hii au uhusiano huu? Ni rahisi kabisa .tukiyatunza mazingira m

wanamke atapata nafasi nzuri ya kupata maji katika umbali mfupi,kutakua na mvua za kutosha ambapo ataweza kufanya shughuli za kilimo ili kuweza kuongeza kipato cha familia na uchumi wa nchi kwa ujumla .Tutunze mazingira kwa ajili ya maendeleo ya mwanamke kwani ukimkomboa mwanamke umekomboa jamii nzima.







First

Toa maoni ili tuweze boresha huduma za taarifa zetu na sio matusi Tafadhari
EmoticonEmoticon